Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:08

Nigeria Yaagiza chanjo dhidi ya Corona. Viongozi wa serikali na madaktari kupewa kipau mbele


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Nigeria inatarajia kupokea chanjo dhidi ya virusi vya Corona mwishoni mwa mwezi huu wa Januari.

Mkuu wa taasisi ya afya ya msingi Faisal Shuaib, amesema kwamba nchi hiyo imepanga kutoa chanjo hiyo kwa asilimia 40 ya watu wote katika awamu ya kwanza mwaka huu.

Asilimia 30 ya watu nchini Nigeria watapewa chanjo dhidi ya Corona mwaka ujao.

Dozi 100,000 za chanjo iliyotengenezwa na kampuni ya Pfizer BioNTech imeagizwa na serikali ya Nigeria kupitia mpango wa kugawana chanjo hiyo unaojulikana kama Covax.

Watakaotangulia kupewa chanjo

Maafisa wa afya walio katika msitari wa mbele katika kupambana na Corona watakuwa wa kwanza kupewa chanjo hiyo, wakifuatiwa na viongozi wa taifa, halafu watu walio katika hatari ya kuambukizwa kisha watu wazee.

Nigeria ina matumaini ya kupata dozi milioni 42 za chanjo dhidi ya Corona.

Shirika la afya duniani lilizindua mpango wa Covax ili kusaidia nchi maskni kupata chanjo dhidi ya Corona wakati kuna wasiwasi kwamba nchi Tajiri huenda zikajitengea chanjo yote.

Afrika kusini yaanza mipango ya kununua chanjo

Nchini Afrika kusini, rais Cyril Ramaphosa amesema kwamba anatarajia utawala wake kununua chanjo hiyo kupitia mpango wa Covax katika robo ya pili yam waka 2021, baada ya kulipa dola milioni 283.

Waziri wa afya wa Afrika kusini Zweli Mkhize amesema kwamba serikali inafanya mazungumzo na kampuni za kibinafsi za kutengeneza chanjo hiyo ili kuhakikisha kwamba inapatikana nchini Afrika kusini mwezi ujao.

Afrika kusini imekumbwa na shinikizo kubwa la kutaka kuanza kutoa chanjo kwa raia wake, baada ya kuripotiwa aina mpya ya virusi vya Corona nchini humo.

Zaidi ya watu milioni 1.1 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Afrika kusini, na karibu 100,000 nchini Nigeria.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington

XS
SM
MD
LG