Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:44

Utawala wa Biden unaongeza kasi ya usambazaji chanjo ya COVID nchi nzima


Mfanyakazi wa huduma ya afya akiandaa chanjo ya COVID-19 huko New York, Marekani, January 29, 2021.
Mfanyakazi wa huduma ya afya akiandaa chanjo ya COVID-19 huko New York, Marekani, January 29, 2021.

Kulingana na taarifa ya White House utawala wa Biden na Harris unaongeza usambazaji wa chanjo ya kila wiki kwa majimbo, makabila na wilaya hadi dozi milioni 10.5 kuanzia wiki hii

Makao makuu ya serikali ya Marekani, White House, imetangaza Jumanne hatua mpya ili kuongeza viwango vya chanjo dhidi ya COVID-19 ikiwemo usambazaji wa chanjo hiyo kwenda maduka yanayouza dawa nchi nzima.

Katika kulipa uzito tangazo la wiki iliyopita ni kwamba utawala wa Biden na Harris utaongeza usambazaji wa chanjo ya kila wiki kwa majimbo, makabila na wilaya hadi dozi milioni 10.5 nchi nzima kuanzia wiki hii, taarifa kutoka White House imesema, ikibainisha kuwa hii ni asilimia 22 kwenye ongezeko la usambazaji wa chanjo tangu Rais Joe Biden aingie madarakani januari 20.

Taarifa pia imesema serikali kuu itayalipa majimbo na wilaya kwa vifaa kama vile barakoa na Gloves wakati Marekani inaendelea kupambana na idadi kubwa ya maambukizi pamoja na vifo vinavyotokana na virusi vya Corona.

XS
SM
MD
LG