Biden, mwenye umri wa miaka 78, anakuwa kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi kutumikia kwa miaka 36 kama seneta wa Marekani na miaka minane nafasi ya makamu rais. Aliapishwa kuitetea Katiba ya Marekani na kuilinda nchi dhidi ya maadui wote, wa kigeni na wa ndani ya nchi. Ilikuwa ni siku yenye baridi na upepo.
Muda mfupi kabla ya hapo, Kamala Harris, seneta wa zamani wa California, jimbo lenye wakazi wengi nchini Marekani, aliapishwa kama makamu rais, na kuwa ni mwanamke mwenye cheo cha juu kuliko wote baada ya karne mbili ya historia ya Marekani. Ni mwenye asili ya Kiafrika na Kihindi.
Katika hotuba yake ya kuapishwa, Biden amesema “Matakwa ya watu yamesikika, na yamezingatiwa. Tumejifunza mara nyingine kuwa demokrasia ni yenye thamani na demokrasia inaweza kuharibika. Katika saa hii, Rafiki zangu, demokrasia imeshinda.”
“Hii ni Marekani ya leo. Hii ni siku ya demokrasia. Siku ya historia na ya matumaini, kuihuisha na kupata ufumbuzi,” ameongeza. Biden pia alisisitiza “umoja ndio mustakbali wa taifa.”
Sherehe za kuapishwa zilishuhudiwa na marais watatu wa zamani –Barack Obama, George W. Bush na Bill Clinton – lakini rais aliyemaliza muda wake Donald Trump alipuuza utamaduni wa miaka 152 wa marais kuhudhuria kuapishwa kwa warithi wao na aliondoka Washington mapema kuelekea katika nyumba yake ya kifahari pwani ya Atlantic huko Florida.