Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:23

Biden atengua katazo lililowekwa na Trump la kusafiri lililolenga Afrika na nchi zenye Waislam wengi


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joseph Biden ametoa amri ya kiutendaji wiki hii kutengua katazo la kusafiri lenye kulenga nchi zenye Waislamu walio wengi na nchi za Kiafrika.

Chini ya amri hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje lazima aamrishe balozi za Marekani na balozi ndogo zianze mchakato wa maombi ya visa huko nyuma zilizuiliwa na katazo hilo katika utaratibu wa kawaida unaofuatwa na ofisi za kutoa visa na tahadhari za COVID-19.

Raia wa Tanzania, Eritrea, Kyrgyzstan, Myanmar (Burma), Nigeria, Sudan hawahusishwi tena na katazo la visa za uhamiaji zilizo tangazwa Januari 2020 na Trump.

Kadhalika kufuatia amri ya kiutendaji hiyo, raia wa Iran, Libya, Korea Kaskazini, Somalia, Syria, Venezuela na Yemen hawatazuiliwa tena kupatiwa visa zisizo kuwa za uhamiaji na/ au visa za uhamiaji, kutokana na katazo la kusafiri lililotolewa na Trump mwaka 2017, na kubadilishwa mara kadhaa huku likipingwa kisheria, na hatimaye kuthibitishwa na Mahakama ya Juu Juni 2018.

Makatazo yote mawili yaliruhusu kuwepo nchi zenye kupewa upendeleo fulani au kuondolewa katika vikwazo hivyo, lakini kiuhakika, upendeleo huo ulikuwa na changamoto kwa nchi hizo kupewa na unaweza kucheleweshwa kwa kipindi kirefu.

Rais wa zamani Donald Trump akiwasili Florida Florida, Jan. 20, 2021.,baada ya kumaliza miaka minne ya utawala wake .
Rais wa zamani Donald Trump akiwasili Florida Florida, Jan. 20, 2021.,baada ya kumaliza miaka minne ya utawala wake .

Uongozi wa Trump ulisema ulikuwa umeweka mfumo wa kutathmini daraja tatu – “iwapo serikali ya kigeni inajihusisha na utaratibu unaoaminika wa kusimamia utambulisho wa raia wake na kubadilishana taarifa husika ; iwapo serikali ya kigeni inabadilishana taarifa za usalama wa kitaifa na usalama wa umma; na iwapo nchi inahatarisha usalama wa kitaifa au usalama wa umma.”

Kushindikana kupima vigezo hivi kulipelekea nchi sita hizo kuingizwa katika orodha ya katazo la kusafiri.

XS
SM
MD
LG