Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:54

Baraza la Seneti latarajiwa kupiga kura kumuidhinisha Jenerali Austin


 Jenerali mstaafu Lloyd Austin (Jim Lo Scalzo/Pool via AP)
Jenerali mstaafu Lloyd Austin (Jim Lo Scalzo/Pool via AP)

Baraza la Seneti la Marekani linatarajiwa kukutana Ijumaa kupiga kura ya kumuidhinisha Jenerali mstaafu Lloyd Austin aliependekezwa na rais Joe Biden kwenye wadhifa wa Waziri wa Ulinzi.

Alhamisi Baraza la Wawakilishi na Seneti walipitisha kanuni ya kisheria kumruhusu Austin kuchukua wadhifa wa waziri wa ulinzi kama raia wa kawaida chini ya miaka 7 tangu ajiuzulu kwenye jeshi la Marekani.

Austin ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Vikosi vya Marekani Mashariki ya Kati na Asia kusini na Kamanda wa Uongozi wa jeshi, akiidhinishwa na Seneti, atakuwa Mmarekani mweusi wa kwanza kuchukua wadhifa wa Waziri wa Ulinzi.

Baraza la Seneti linatarijiwa pia kumuidhinisha Balozi wa zamani William Burns aliependekezwa na Rais Biden kuongoza idara ya Ujasusi ya Marekani, CIA.

XS
SM
MD
LG