Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:06

Utawala wa Biden wajikita siku ya kwanza kupata majibu ya serikali kuu


Rais Joe Biden akisaini amri za kiutendaji ofisini White House, Washington, DC, mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa 46 wa Marekani. January 20, 2021. REUTERS/Tom Brenner
Rais Joe Biden akisaini amri za kiutendaji ofisini White House, Washington, DC, mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa 46 wa Marekani. January 20, 2021. REUTERS/Tom Brenner

Rais wa Marekani Joe Biden na Makamu Rais Kamala Harris wameweka mkazo mkubwa siku yao ya kwanza kamili ofisini juu ya majibu ya serikali kuu katika kupambana na virusi vya corona.

Biden alitarajiwa kuzungumza Alhamisi juu ya mipango ya utawala wake na kutia saini maagizo ya kiutendaji na hatua nyingine zinazo husiana na kupambana na COVID-19.

Wote Biden na Harris wanatarajia kuarifiwa na timu yao ya kupambana na Corona, ikiwa ni pamoja na kupata habari kuhusu hali ya sasa ya mipango ya chanjo inayo fanyika kote nchini.

Biden aliweka lengo la kuongeza chanjo mwanzoni mwa kipindi cha utawala wake ili kutoa chanjo milioni 100 katika siku 100 za kwanza.

XS
SM
MD
LG