Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:00

Trump amwandikia Biden ujumbe na kuuacha white house


Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump amefuata angalau utamaduni mmoja kama ilivyo kawaida na marais wanaondoka madarakani.

Maafisa wa white house wanasema kwamba Trump amemwandikia ujumbe rais Joe Biden.

Naibu wa maswala ya habari katika white house Judd Deere, hata hivyo hajasema yaliyomo kwenye ujumbe wa Trump kwa Biden, akisema kwamba hizo ni kanuni za mawasiliano ya siri kati ya marais.

Trump amekataa kabisa kuutambua hadharani ushindi wa Joe Biden na wala hakutaja jina la Biden katika hotuba yake ya mwisho ya kuondoka madarakani.

Trump amekosa kutimiza tamaduni za urais Marekani, ikiwemo kukataa kuhuduria sherehe ya kuapishwa kwa Joe Biden.

Trump hakumwalika Biden katika ikulu ya white house kwa mkutano kati ya rais anayeondoka na ayeingia madarakani ilivyo kawaida.

XS
SM
MD
LG