Rais wa Marekani anayeondoka madarakani Donald Trump, amewasamehe zaidi ya watu 140 wlaiokuwa wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali ya uhalifu, saa chache kabla ya kuondoka white house.
Miongoni mwa waliopata msamaha wa rais ni aliyekuwa msimamizi wa mikakati ya Trump Steve Bannon, aliekuwa anakabiliwa na mashataka ya kulaghai watu mamilioni yad ola.
Wengine ni wanamuziki, waliokuwa wabunge, watu walio karibu san ana Trump Pamoja na watu kutoka kwa familia yake.
Orodha hiyo ya watu ambao wamepata msamaha wa rais imetolewa alfajiri hii leo, na inakuja siku chache baada ya Trump kutoa msamaha kwa watu walio karibu naye, waliokuwa wamefunguliwa mashtaka ya uhalifu kutokana na uchunguzi uliofanywa na FBI kuhusu Russia kuingilia kati uchaguzi mkuu wa Marekani mwa kwama 2016.
Watu wengine waliosamehewa walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya uhalifu na kumiliki silaha kinyume cha sheria Pamoja na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Mwanamuziki Dwayne Michael Carter maarufu Lil Wayne, na Kodak Black ambao walikuwa wanakabiliwa na makosa ya kumiliki bunduki kinyume cha sheria, ni miongoni mwa watu ambao wamepata msamaha wa Trump.