Kaimu mwanasheria mkuu wa Marekani Jeffrey Rosen ametangaza kwamba atajiuzulu hii leo, baada ya kuongoza idhara hiyo kwa mda mfupi chini ya utawala wa rais anayeondoka madarakani Donald Trump.
Rosen aliteuliwa kuwa kaimu wa mkuu wa sheria mwezi Desemba tarehe 23 baada ya Bill Barr kujiuzulu.
Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba Trump alikuwa anamshinikiza Rosen, kuunda tume maalum kuchunguza madai ya wizi wa kura katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba mwaka uliopita.
Rosen, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba lengo lake kubwa ofisini lilikuwa kufanya kazi kulingana na sheria na ukweli.
Msemaji wa idhara ya sheria amesema kwamba Rosen hajaunda tume yoyote wakati akiwa ofisini.
Alishutumu uvamizi wa wafuasi wa Donald Trump bungeni, Januari tarehe 6, na maafisa wake kuanza uchunguzi kuwakamata watu waliohusika.