Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:20

COVID-19 : Maambukizi duniani yafikia milioni 116


Wagonjwa wa COVID-19 wakiwa katika uwanja wa mpira uliojengwa hospitali huko Santo Andre, nje ya mji Sao Paulo, Brazil, Alhamisi, March 4, 2021. (AP Photo/Andre Penner)
Wagonjwa wa COVID-19 wakiwa katika uwanja wa mpira uliojengwa hospitali huko Santo Andre, nje ya mji Sao Paulo, Brazil, Alhamisi, March 4, 2021. (AP Photo/Andre Penner)

Kituo cha kufuatilia maambukizi ya virusi vya Corona cha Johns Hopkins kimerekodi maambukizi zaidi ya milioni 116 ya virusi vya corona duniani.

Kituo cha kufuatilia maambukizi ya virusi vya Corona cha Johns Hopkins kimerekodi maambukizi zaidi ya milioni 116 ya virusi vya corona duniani.

Marekani inaelekea kufikia maambukizi milioni 30, ikifuatiwa na India yenye maambukizi milioni 11 na Brazil milioni 10.8.

Mapema wiki hii, Rais wa Brazili Jair Bolsonaro alitoa tamko liloonyesha kutowajali wananchi wenzake waliokuwa hawajafurahishwa na namna rais alivyokabiliana na janga hilo.

“Acheni kupinga na kulalamika,” rais alisema. “Mpaka lini mtaendelea kulalamika?” Bolsonaro alikuwa anazungumza katika jimbo la Goias, Brazil, ambako takriban watu 9,000 walifariki.

Ni Marekani peke yake ndio ina vifo zaidi vya COVID kuliko Brazil. Kwa mujibu wa Hopkins, Marekani ina zaidi ya vifo 522,000 vya COVID-19, wakati Brazil imeripoti zaidi ya vifo 262,000.

Idara ya takwimu ya Russia imesema Ijumaa zaidi ya Warussia 200,000 waliogundulika na maambukizi ya COVID-19 wamefariki, zaidi ya mara mbili ya idadi inayotolewa na kikosi kazi cha serikali kinacho shughulikia virusi vya corona.

Idadi iliyotolewa Ijumaa na Rosstat, idara ya serikali ambayo inachapisha takwimu sio mara kwa mara, imesema ilikuwa imesajili vifo 200,432 hadi mwezi Januari. Takwimu hizo ni pamoja na takriban watu 70,000 waliokuwa na maambukizi ya virusi hivyo wakati wanafariki, lakini sababu kuu ya vifo vyao haijazingatia kuwa ni COVID-19.

Kwa kutumia takwimu za Rosstat, Russia itakuwa ni ya tatu yenye vifo vingi vya COVID-19 duniani, ikiifuatia Marekani na Brazil

Rosstat pia imeripoti Ijumaa kuwa Russia imesajili zaidi ya vifo 394,000 tangu kuanza kwa janga hilo hadi kufikia mwisho wa Januari kuliko katika kipindi kilichopita --- ikionyesha kuwa vifo vinavyotokana na virusi vya corona nchini humo huenda vikawa juu zaidi.

Katika maendeleo mengine Ijumaa, Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema wachunguzi waliokuwa wamefanya ukaguzi nchini China kutafiti asili ya virusi vya COVID-19 watatoa ripoti ya walichogundua ifikapo katikati ya mwezi Machi.

Marion Koopmans, kulia, na Peter Ben Embarek, katikati, wa Shirika la Afya Duniani wakiangana na wanasayansi wa china wenyeji wao Liang Wannian, kushoto, baaday ya uchunguzi wa pamoja wa WHO-China wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari baada ya ujumbe wa WHO kukamilisha shughuli zao Wuhan, China,
Marion Koopmans, kulia, na Peter Ben Embarek, katikati, wa Shirika la Afya Duniani wakiangana na wanasayansi wa china wenyeji wao Liang Wannian, kushoto, baaday ya uchunguzi wa pamoja wa WHO-China wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari baada ya ujumbe wa WHO kukamilisha shughuli zao Wuhan, China,

Peter Ben Embarek, aliyeongoza ujumbe huo wa watafiti, amefafanua katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kuhusu virusi vya corona Ijumaa mjini Geneva kuwa ripoti ya awali haitatolewa kama ilivyokuwa imetangazwa.

“Kwanza kabisa, napenda kufafanua, hakukuwa na mpango wa kutoa ripoti ya awali,” amesema Embarek. “Ilitarajiwa tutaweza kutoa muhtasari,” lakini “ Mkurugenzi mkuu [Tedros Adhanom Ghebreyesus] atapokea ripoti kutoka timu ya wachunguzi siku za karibuni na atajadili mapendekezo.”

Jarida la Wall Street liliripoti Alhamisi kuwa timu ya WHO iliamua kutotoa ripoti ya awali “ kufuatia mvutano uliojiri kati ya Beijing na Washington.”

Kundi jingine la wanasayansi limeitaka WHO kufanya uchunguzi mpya juu ya chanzo cha COVID-19. Wana sayansi hao wametaka uchunguzi huo mpya katika barua yao ya wazi iliyotolewa Alhamisi wakieleza kuwa timu ya WHO “ haikuwa na mamlaka, uhuru na ruhusa muhimu ya kufanya uchunguzi kamili usiokuwa na masharti.”

Wana sayansi hao pia wameeleza katika barua yao kwamba wachunguzi wa WHO waliokwenda China walikuwa wanafuatana na wanasayansi wenzao wa China.

Maambukizi ya kwanza ya COVID-19 yaliripotiwa katika mji wa Wuhan nchini China Disemba 2019.

XS
SM
MD
LG