Ndege iliyobeba dozi 600,000 za chanjo za AstraZeneca kutoka Chuo Kikuu cha Oxford ziliwasili leo Jumatano katika mji mkuu, Accra.
Kulingana na taarifa ya pamoja kutoka WHO na UNICEF, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Dharura kwa Watoto chanjo hizo zilitengenezwa na Taasisi ya Serum ya India, mtengenezaji mkubwa wa chanjo duniani.
Chanjo zilizopelekwa Ghana zilinunuliwa kupitia Kituo cha Upatikanaji wa Chanjo cha COVID-19, au COVAX, mradi uliozinduliwa na WHO kwa kushirikiana na Coalition for Epidemic Preparedness Innovations na Gavi, The Vaccine Alliance.
Shirika hili lilianzishwa na wahisani Bill na Melinda Gates kuwapatia chanjo watoto katika nchi masikini zaidi duniani.
Mradi huo unanunua chanjo kwa msaada wa nchi tajiri na kuzisambaza kwa usawa kwa nchi zote. Rais wa Marekani Joe Biden aliahidi dola bilioni 4 kwa mradi huo wa COVAX wiki iliyopita.