Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:30

COVID-19 : WHO yaitaka Tanzania kutekeleza kanuni za afya kudhibiti maambukizi


Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Shirika la Afya Duniani(WHO) limeitaka Tanzania kutekeleza kanuni za afya ya jamii ambazo zinajulikana zinafanya kazi katika kuzuia mfululizo wa maambukizi, na kujiandaa kupata chanjo, taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus imeleza.

Taarifa hiyo ya Jumamosi imesema Watanzania kadhaa wanaosafiri katika nchi jirani na sehemu nyingine wamegundulika wana maambukizi ya virusi vya COVID-19 baada ya kupimwa.

"Hii inaonyesha kuna haja kwa Tanzania kuchukua hatua za haraka kuwalinda watu wake na kuzilinda jamii nyingine katika nchi jirani na ulimwenguni. Hali hii inatia wasiwasi mkubwa. Ninarejea wito wangu kwa Tanzania kuanza kuripoti maambukizi ya COVID-19 na kushirikiana kutoa takwimu,” amesema mkurugenzi huyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa COVID-19 ni ugonjwa ambao unaweza kuleta athari mbaya sana na hata kifo. Mamlaka za kitaifa kila mahali lazima wafanye kila kinachowezekana kuwalinda watu na kuokoa maisha. WHO iko tayari kuwasaidia kukabiliana na virusi hivyo hatari.

Kadhalika Mkurugenzi Mkuu ametuma salamu za rambirambi akisema : “Tunawapa pole ndugu zetu wa Tanzania kwa vifo vya viongozi wa juu Tanzania na pia Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali.”

“Mwisho wa mwezi Januari, niliungana na Dr Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO wa Eneo la Afrika kuisihi Tanzania kuchukua hatua zaidi za afya ya umma dhidi ya COVID-19 na kujiandaa na chanjo. Pia nilihamasisha juu ya kubadilishana takwimu kwa taarifa zilizojitokeza za maambukizi ya COVID-19 kati ya wasafiri,” amesema Mkurugenzi Adhanom.

“Tangu wakati huo nimezungumza na mamlaka kadhaa nchini Tanzania lakini WHO mpaka sasa haijapokea taarifa zozote kuhusu hatua zinazochukuliwa na Tanzania kukabiliana na janga hilo la corona,” ameeleza.

XS
SM
MD
LG