Uingereza imepiga marufuku wasafiri kutoka Tanzania na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuingia nchini humo kuanzia leo ijumaa, ikiwa ni hatua ya kudhibithi maambukizi ya aina mpya ya virusi vya Corona.
Kituo cha Kudhibithi magonjwa Afrika, kimesema alhamisi kwamba kiwango cha vifo kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona Afrika kimefikia asilimia 2.5.
Kiwango hicho kipo juu zaidi kuliko asilimia 2.2 ambacho ni kiwango cha wastan kote duniani.
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeorodheshwa miongoni mwa nchi 21 za Afrika zenye viwango vya vifo vya zaidi ya asilimia 3.
Mamlaka nchinio Tanzania huwa haitoi taarifa zozote kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.
Rais wa Tanzania John Magufuli alitangaza kwamba Tanzania haina maambukizi ya virusi vya Corona kabisa lakini shirika la afya duniani limeelezea wasiwasi kuhusu mikakati ya nchi hiyo kupambana na janga hilo la afya.