Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:30

Maalim Seif afariki baada ya kuugua Corona


Marehemu Seif Sharif Hamad
Marehemu Seif Sharif Hamad

Maalim Seif Sharif Hamad, Kiongozi aliyeongoza upinzani wa Zanzibar kwa karibu miongo mitatu amefariki Jumatano katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam baada ya kuugua ugonjwa wa COVID-19 kwa wiki tatu.

Maalim Seif alikuwa mmoja kati ya wanasiasa wakongwe na mashuhuri wa Zanzibar na Tanzania aliyegombania mara tano kiti cha urais na kushindwa, lakini kila mara alidai aliibiwa ushindi.

Kiongozi huyo wa upinzani anaingia katika historia kwa kuwa miongoni mwa wagombea wa upinzani wa nchi nyingi za Afrika walioibiwa ushindi mara kadhaa.

Maisha ya Maalim Seif

Maalim Seif aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar akiwa ni miongoni mwa Wazanzibari waliozuiliwa kuendelea na masomo ya juu kwa karibu miaka 9 kwa kukataa kufanya kazi ya umma kutokana na kuondoka kwa maafisa wa utawala wa kikoloni wa Uingereza 1964, alihitimu na kupata shahada ya kwanza ya sayansi ya siasa kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Muda mfupi baada ya kuhitimu masomo ya juu aliingia katika siasa akiwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na kuteuliwa waziri wa elimu, akiwa pia mbunge katika bunge la taifa la Tanzania. Pia aliwahi kuwa kiongozi katika Umoja wa Vijana wa CCM, Zanzibar.

Mshauri wake wa karibu na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha ACT-Wazalendo, Ismail Jussa anasema Maalim Seif alikuwa na nguvu katika siasa kwa miaka 43 kutokana na “kuungwa mkono na wanananchi waliowengi wa Zanzibar.

Jussa anaeleza : "Lakini licha ya umashuhuri wake Maali Seif alishindwa katika uchaguzi tangu mwaka 1995 hadi uchaguzi wa mwisho wa 2005.

Mwaka 2000 ndio ulishuhudia ghasia kubwa baada ya kushindwa na kwenye maandamano ya januari 2001 wafuasi 45 wa CUF waliuliwa na wengine kukimbia uhamishoni. Makubaliano yaliyo fahamika kama muafaka yalifikiwa na kufanya mageuzi ya katiba juu ya kushirikiana madaraka. Lakini baada ya awamu moja makubaliano hayakuendelea na Maalim kuendelea kugombania kiti cha rais.

Jussa anasema huwenda kasoro yake kubwa ilikuwa ni kutaka amani na majadiliano na kule kwamba anapendwa na Wazanzinbari.

Baadhi ya wachambuzi wanasema Maalim Seif hakutayarisha vijana kuchukua nafasi yake licha ya kwamba anapendwa sana na Wananchi.

Dk Mzuri Issa mchambuzi wa masuala ya kisiasa Zanzibar anasema ni kweli maalim ni mwanasiasa anaependwa na mwenye haiba ya kutosha lakini mambo yamebadilika.

Lakini Jussa anapinga suala la kwamba kiongozi huyo hajawatayarisha vijana kuchukua nafasi za uongozi.

XS
SM
MD
LG