Mwenyekiti Maalim Seif Sharif Hamad amekubali nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais baada ya kuteuliwa na Rais Hussein Ali Mwinyi, na kutarajiwa kuapishwa rasmi siku ya Jumanne.
Chama hicho kipya cha upinzani hakikubaliana na matokeo ya uchaguzi wa bunge na wa baraza la wawakilishi, wala hakikutambua matokeo ya uchaguzi wa Rais.
Hii ni mara ya pili kwa Sharif Hamad kuchukua nyadhifa hiyo ambapo mara ya kwanza ilikua mwaka 2010 hadi 2015, wakati kulikua pia na utata mkubwa kwenye uchaguzi ulosababisha vifo na mamia ya watu kukimbia kutoka visiwani humo.
Akizungumza na Sauti ya Amerika akiwa hospitali mjini Nairobi siku ya Jumatatu, mwanachama muandamizi kwenye Kamati Kuu ya chama cha ACT-Wazalendo, Ismail Jussa amesema, "kwanza ni uwamuzi unaotokana na katika ya visiwa hivyo inayotaka kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Lakini umuhimu zaidi anasema, "ni uwamuzi ulochukuliwa kwa pamoja na viongozi wa chama baada ya kusikiliza maoni ya wanachama katika majimbo sote ya Unguja na Pemba.
Kabla ya kuchukua uwamuzi wa kujiunga na serikali chama cha ACT kilipinga matoneo na kusema hakitashiriki kwenye serikali.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa Absalom Kibanda, anasema "uwamuzi huu wa sasa wa ACT-Wazalendo umetuonesha baadhi yetu kwamba chama hicho kimejifunza, ama kwa makosa yake ya 2015, ambapo waliamua kususia uchaguzi maalum na uteuzi wa baraza la wawakilishi, na mwishowe wakajikuta wanapoteza katika majukwa ya kushiriki katika maamuzi na uwongozi."
Jussa na Kibanda wanasisitiza kwamba, uamuzi huo haujasaliti dhamira na małego ya wanachama wao na wapigaji kura, kama jinsi wakosowaji wanavyo dai.
Jussa anasema makubaliano hayo yatawawezesha kutetea vilivyo malalamiko yote ya kasoro kwenye uchaguzi, kutaka uchunguzi kufanyika kutokana na kunyanyaswa na kupigwa kwa wanachama na hatimae kushiriki katika kupanga mustakbali mzuri zaidi wa uchaguzi na utawala visiwani Zanzibar. .