Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 19:40

Chama cha Chadema chasema hakijui aliowateua wabunge maalum walioapishwa na Ndugai


Halima Mdee - mmoja wa wabunge maalum wa Chadema walioapishwa bungeni Jumanne Nov 24 2020
Halima Mdee - mmoja wa wabunge maalum wa Chadema walioapishwa bungeni Jumanne Nov 24 2020

Chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema, kimefutilia mbali orodha ya wabunge 19 wa viti maalum walioapishwa bungeni jijini Da-es-salaam, kikisema kwamba hakina taarifa kuhusu uteuzi huo.

Katibu mkuu wa chama cha Chadema John Mnyika ameandika ujumbwe wa twiter ambao umesambazwa na ukuraswa wa twiter wa chama kwamba “kamati kuu ya chama cha chadema haijafanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum mpaka sasa. Hivyo hakuna orodha iliyopelekwa na katibu mkuu kwa tume ya uchaguzi NEC.” Ujumbe huo umeendelea kusema kwamba chama cha Chadema kimapata taarif akwamba wahusika waliotengeneza orodha hiyo “wanataka kughushi Saini na orodha ili tume ya uchaguzi ifanye uteuzi haramu na bunge litabariki.”

Katika mahojiano na idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Amerika matangazo ya jioni (Novemba 24 2020) katibu mkuu wa chama cha Chdema Mnyika John, amesema kwamba hana taarifa yoyote kuhusu wabunge walioapishwa na spika Ndugai na kwamba uteuzi wao ni jambo geni kwa maafisa wa chama.

Baadaye ameandika kwa twiter kwamba “tunafuatilia yanayojiri katika ofisi ya spika wa bunge la Tanzania na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua.” Amemalizia kwa kusema kwamba “turejee kwenye mjadala kuhusu uchaguzi.

Viti maalum bungeni

Kulingana na sheria, Chama cha Chadema kinastahili kupata viti maalum 19 kulingana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwezi uliopita.

Idadi ya viti maalum inafikiwa kutokana na idadi ya kura alizopata mgombea wa urais wa kila chama.

Kulingana na tume ya uchaguzi ya Tanzania, mgombea wa urais wa chama cha Chadema Tundu Lissu, alipata kura milioni 1.9.

Chama hicho kilishinda kiti kimoja cha bunge.

Rais John Magufuli wa chama cha CCM alipata kura milioni 12.5.

Kulingana na hesabu hiyo, chama cha Chadema kinastahili kutengewa viti maalum vya bunge 19, na CCM kutengewea viti 95.

Hata hivyo, chama cha Chadema na ACT wazalendo, vimekataa matokeo ya uchaguzi mkuu, vikidai kwamba kulifanyika udanganyifu katika hesabu ya kura.

Wabunge maalum wa Chadema walioapishwa

Kati ya wabunge 19 walioapishwa na spika Job Ndugai katika bunge la Dodoma, 14 ni waliokuwa wabunge katika bunge la 11. Wengine 5 ni sura mpya bungeni.

Wabunge hao ni Halima Mdee, Naghenjwa Kaboyoka, Esther Matiko, Esther Bulaya, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Kishoa David, Anatropia Theonest, Salome Makamba, Conchesta Rwamlaza, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo.

Wengine ni Agnes Kaiza, Asia Mohamed, Nusrat Hanje, Felister Njau na Stella Fiayo.

Idadi ya wabunge wa Chadema

Chama cha Chadema sasa kina wabunge 20 baada ya kuapishwa kwa wabunge wake maalum 19.

Aida Khenan ndiye mbunge pekee wa chama hicho aliyeshinda katika uchaguzi wa mwezi uliopita. Alimshinda mgombea wa chama cha CCM kwa kura 1,254 katika eneo bunge la Nkasi kaskazini, Rukwa. Aliapishwa wiki mbili zilizopita.

Spika wa bunge Job Ndugai amesema kwamba alipokea majina ya wabunge hao wa viti maalum kutoka kwa tume ya uchaguzi NEC.

Kupitia ukurasa wake wa twiter, chama cha Chadema kimeitisha kikao na waandishi wa habari Jumatano Novemba 25 2020 kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu hatua hiyo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG