Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:27

Maalim Seif apumzishwa hospitalini kutokana na COVID-19


Makamu wa Rais wa kwanza Seif Sharif Hamad
Makamu wa Rais wa kwanza Seif Sharif Hamad

Chama cha ACT Wazalendo nchini Tanzania kimesema kuwa Mwenyekiti wake wa Taifa Maalim Seif Sharif Hamad na mkewe Awena pamoja na wasaidizi wake kadhaa wa karibu wamepata maambukizi ya COViD-19 baada ya kufanyiwa vipimo.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama cha ACT Wazalendo hali ya Maalim Seif na mkewe zinaendelea vyema kabisa.

Kadhalika ACT Wazalendo imerejea wito wake kwa Watanzania wote kuendelea kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi madaktari wamemshauri Maalim Seif kuendelea kuwa chini ya uangalizi maalum katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu dhidi ya maradhi hayo.

Maalim Seif kuanzia Ijumaa jioni alilazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja , mjini Unguja, Zanzibar ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

Uongozi wa ACT Wazalendo unawataka wanachama wake, Zanzibar na Tanzania bara kumuombea dua Maalim Seif katika kipindi hiki cha kuugua kwake, ili aweze kupona kwa haraka na kurudi kuendelea na majukumu yake.

XS
SM
MD
LG