Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:09

Afrika Kusini yasitisha kwa muda kutoa chanjo ya AstraZeneca


Chanjo ya AstraZeneca (AP Photo/Frank Augstein)
Chanjo ya AstraZeneca (AP Photo/Frank Augstein)

Afrika Kusini imesitisha kwa muda kampeni yake ya chanjo dhidi ya COVID-19 Jumapili baada ya utafiti mpya kubaini kuwa chanjo ya AstraZeneca haifanyi kazi vizuri dhidi ya aina mpya ya virusi vinavyopatikana nchini humo.

Shirika la Afya Duniani - WHO linafanya mkutano Jumatatu kuhusu maendeleo ya hivi karibuni nchini Afrika Kusini.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus

Utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Witwatersrand huko Johannesburg na bado haujafanyiwa tathmini ulihitimisha kuwa chanjo ya Uingereza ilitoa tu kinga ndogo dhidi ya aina za wastani za ugonjwa unaosababishwa na aina tofauti ya virusi huko Afrika Kusini, kwa vijana.

Habari hiyo ilikuwa pigo kwa Afrika Kusini, ambayo imeshuhudia zaidi ya watu 46,000 wakifariki kutokana na virusi. Ilikuwa imepanga kuanza kuchanja watu wake na dozi milioni moja za chanjo ya AstraZeneca katika siku zijazo. Lakini utafiti uligundua kuwa chanjo hiyo ilikuwa na ufanisi wa asilimia 22 tu katika visa vya wastani vya aina ya ugonjwa huo wa Afrika Kusini.

Utafiti huo haukukagua athari ya chanjo dhidi ya visa vyenye athari kubwa vya ugonjwa huo. Aoina hii ya ugonjwa imepatikana katika nchi nyingine 32 ikiwa ni pamoja na hapa Marekani.

XS
SM
MD
LG