Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:30

Mkuu wa WHO anayalaumu mataifa tajiri yanadumaza juhudi za chanjo ya Corona


Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza kutoka Geneva, Feb. 21, 2021.
Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza kutoka Geneva, Feb. 21, 2021.

Tedros amesema baadhi ya nchi zenye kipato cha juu zinaingia mikataba na watengenezaji wa chanjo ambapo inadhoofisha mikataba ambayo COVAX imefanya na kampuni hizo hizo za kutengeneza madawa

Mkuu wa shirika la afya Duniani-WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, Jumatatu amesema baadhi ya mataifa tajiri Duniani yanadumaza juhudi zinazofanywa na shirika lake na marafiki zake kupata chanjo kwenda mataifa maskini sana Duniani.

Tedros alishiriki katika mkutano wa pamoja kwa njia ya video na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier wakizungumzia kuhusu mpango wa chanjo ya kimataifa uliowezeshwa na WHO na COVAX uliobuniwa kupata na kusambaza kwa usawa chanjo za COVID-19 kote Duniani.

Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkuu wa WHO
Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkuu wa WHO

Akizungumza kutoka makao makuu ya WHO mjini Geneva, Tedros amesema baadhi ya nchi zenye kipato cha juu zinaingia mikataba na watengenezaji wa chanjo ambapo inadhoofisha mikataba ambayo COVAX imefanya na kampuni hizo hizo ikipunguza idadi ya dozi ambazo COVAX inaweza kununua.

Hata hivyo Ghebreyesus hakuzitaja nchi hizo. Mkuu huyo wa WHO amesema anahakikisha kuwa kuna chanjo za kutosha huku zikishirikisha mataifa maskini sana duniani ili kusaidia kila mtu.

XS
SM
MD
LG