Rwanda imesema Jumapili imeanza kutoa chanjo ya COVID-19 na chanjo ndogo zilizopatikana kupitia washirika wa kimataifa ambao hawakutajwa na kusema mpango huo umeanza na wafanyakazi wa huduma ya afya walio kwenye mstari wa mbele.
Rwanda imekua ikikabiliana na ongezeko la maambukizi ya COVID-19 ambayo yalipelekea serikali kuchukua kwa mara nyingine masharti makali kwa kufunga shughuli zote katika mji mkuu Kigali.
Viongozi walipiga marufuku ya kuingia ndani na kutoka nje ya mji wa Kigali isipokuwa huduma muhimu na watalii.
Katika ujumbe wa Twitter, wizara ya afya ya Rwanda imesema mpango wa kitaifa wa chanjo umeanza kwa kuchanja makundi ya watu walio katika hatari hususani wafanyakazi wa huduma ya afya, wakipewa chanjo ya COVID-19 iliyoidhinishwa na WHO na kupatikana kupitia ushirikiano wa kimataifa kwa viwango vidogo.