Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:54

Afrika kusini imeingia mkataba wa chanjo ya Covid na Johnson &Johnson


Chanjo ya COVID-19 ya Johnson &Johnson
Chanjo ya COVID-19 ya Johnson &Johnson

Afrika kusini ndilo taifa linalotaabika sana barani Afrika kutokana na janga la Corona likirekodi nusu ya vifo vyote vya COVID-19 katika bara hilo na zaidi ya theluthi moja ya maambukizi yaliyoripotiwa katika bara zima la Afrika

Afrika kusini imesaini mkataba na kampuni ya Johnson and Johnson ili kununua dozi millioni 11 za chanjo ya COVID-19 na italegeza masharti ya kupambana na janga la Corona kutokana na kupungua kwa kesi mpya, Rais Cyril Ramaphosa amesema Jumapili.

Afrika kusini ndilo taifa linalotaabika sana barani Afrika kutokana na janga la Corona likirekodi nusu ya vifo vyote vya COVID-19 katika bara hilo na zaidi ya theluthi moja ya maambukizi yaliyoripotiwa katika bara zima la Afrika.

Lakini maambukizi ya kila siku yalishuka chini ya elfu mbili kutoka kiwango cha elfu ishirini kwa siku kwa mwezi uliopita wakati wa wimbi la pili la maambukizi ya virusi vya corona.

Rais Cyril Ramaphosa akipatiwa chanjo ya COVID ya Johnson &Johnson mjini Cape Town
Rais Cyril Ramaphosa akipatiwa chanjo ya COVID ya Johnson &Johnson mjini Cape Town

Rais Ramaphosa amesema katika hotuba iliyopeperushwa kwenye televisheni kwamba dozi millioni mbili na laki nane za chanjo ya Johnson and Johnson zitatolewa katika robo ya pili na zilizobaki zitasambazwa baadaye mwaka huu.

Kiongozi huyo wa Afrika kusini amesema dozi millioni ishirini za chanjo za Pfizer zimekwisha tengwa, dozi millioni 12 zitatoka kwenye mradi wa ushirika wa COVAX wa shirika la afya duniani-WHO.

Kwa jumla nchi ina lengo la kuchanja watu millioni 40 sawa na theluthi mbili ya raia wote wa Afrika kusini.

XS
SM
MD
LG