Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:07

Moderna yasema iko tayari kufanya majaribio ya chanjo dhidi ya virusi vipya


Chanjo ya Moderna COVID-19 Feb. 19, 2021, in Oklahoma City. (AP Photo/Sue Ogrocki)
Chanjo ya Moderna COVID-19 Feb. 19, 2021, in Oklahoma City. (AP Photo/Sue Ogrocki)

Kampuni ya Marekani ya Moderna inayo tengeneza chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 inasema iko tayari kufanya majaribio ya chanjo dhidi ya virusi vipya vya corona.

Chanjo hiyo ya majaribio iliyo ongezwa nguvu kupambana na virusi vipya vya Corona, ambavyo viligunguliwa kwanza huko Afrika Kusini.

Utafiti wa awali unaonyesha kwamba chanjo yake ya kwanza iliyo kwisha idhinishwa na Marekani na Umoja wa Ulaya haina nguvu za kutosha kupambana na aina mpya ya virusi vilivyo gunduliwa hivi sasa katika takriban nchi 40.

Kampuni hiyo inasema iko tayari kufanya majaribio kwa binadamu kwa kutumia mikakati mbali mbali kuona ni ipi ina kinga nzuri zaidi.

Moderna inasema majarbio hayo mapya yatafuatilia pia jinsi kinga za mwili za watu waliokwisha chanjwa zinavyo kabiliana na chanjo ya awali pamoja na wale wanaopewa chanjo mpya.

XS
SM
MD
LG