Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:47

Rais Biden ameomboleza vifo vya wamarekani Laki tano kutokana na Corona


Rais Biden na mkewe Jill Biden wakiomboleza vifo vya wamarekani Laki tano kutokana na Corona
Rais Biden na mkewe Jill Biden wakiomboleza vifo vya wamarekani Laki tano kutokana na Corona

Rais Biden alitoa wito kwa taifa kuungana nae katika wakati wa ukimya katika sauti ya chini sana alielekeza matamshi kwa wale ambao wamepoteza wapendwa wao kutokana na virusi vya COVID-19

Rais wa Marekani Joe Biden, Jumatatu jioni alitembea kwenye upande wa pili wa jengo la White House uliopambwa kwa bendera nyeusi pamoja na mishumaa 500 ikiwa ishara wakati taifa linaomboleza vifo laki tano kwa sababu ya COVID-19.

Pembeni ya Rais Biden alikuwepo mkewe Jill Biden na Makamu Rais Kamala Harris pamoja na mumewe Doug Emhoff. Wote walisimama kimya wakati bendi ya Marine Corps ikipiga wimbo wa “Amazing Grace”.

Muziki ulipomalizika Rais Biden ambaye ni mkatoliki muumini mwenye kawaida ya kwenda kanisani alitoa ishara ya msalaba. Dakika chache kabla, kwenye ukumbi wa Cross Hall ghorofa ya kwanza ya White House, Rais Biden alitoa wito kwa taifa kuungana nae katika wakati wa ukimya katika sauti ya chini sana alielekeza matamshi kwa wale ambao wamepoteza wapendwa wao kutokana na virusi vya COVID-19.

XS
SM
MD
LG