Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:19

Maelfu nchini Myanmar waandamana kupinga mapinduzi ya kijeshi


Maandamano Myanmar kupinga mapinduzi ya kijeshi.
Maandamano Myanmar kupinga mapinduzi ya kijeshi.

Maelfu ya watu wamejitokeza mitaani nchini Myanmar Jumapili kwa siku ya pili kupinga mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopita na kutaka kuachiwa kwa kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia Aung San Suu Kyi.

Aung San Suu Kyi.
Aung San Suu Kyi.

Maandamano yaliyo anza sehemu mbalimbali yaliungana huko eneo la Sule Pagoda, katikati ya jiji.

"Mapinduzi ya kijeshi ni ukiukaji wademokrasia na haki za binadamu. Pia ni kebehi kwa nia ya watu. Ndiyo maana tunapinga mapinduzi hayo ya kijeshi,” mmoja wa viongozi wa waandamanaji, Aung San Hmaine, ameiambia idhaa ya Burma katika Sauti ya Amerika. “Ni muhimu kuheshimu matokeo ya uchaguzi. Ndio maana tumejitokeza hapa, kuuandamana.”

Jeshi la Myanmar likiwa barabarani wakati wa maandamano.
Jeshi la Myanmar likiwa barabarani wakati wa maandamano.

Mikusanyiko mikubwa imeripotiwa katika miji mingine pia Jumapili.

Wakati maandamano hayo yakiongezeka siku moja kabla Jumamosi, mamlaka nchini Myanmar ilikuwa imekata mawasiliano ya huduma ya intaneti lakini yamerejeshwa siku ya Jumapili.

Wengi kati ya waandamanaji walikuwa wakiimba “Maisha marefu kwa Mama Suu,” wakikusudia kiongozi aliyepinduliwa Suu Kyi, na, “ Hatutaki udikteta wa kijeshi.” Waandamanaji wengine walinyanyua vidole vitatu kutoa ishara, ikiwa ni alama ya kukataa utawala wa kidikteta katika filamu ya “Hunger Games.”

Utawala wa kijeshi uliochukua madaraka Myanmar tangu Jumatatu iliyopita kwa kumweka kizuizini Suu Kyi, ambaye ndiye kiongozi mstahiki wa nchi hiyo, na kuwekwa kizuizini kwa vingozi wengine waandamizi wa serikali. Suu Kyi anaendelea kushikiliwa nyumbani katika makazi yake rasmi huko Naypyitaw, kulingana na msemaji wa chama Kyi Toe.

Suu Kyi anakabiliwa na mashtaka ya kuingiza kinyume cha sheria na kutumia aina ya radio za mawasiliano walkie-talkie zilizo kuwa hazijasajiliwa zilizo gunduliwa wakati wa upekuzi uliofanywa nyumbani kwake katika mji mkuu wa Naypyitaw.

Jeshi la Myanmar lililotwaa madaraka kwa nguvu limesema hali ya dharura iliyotangazwa, itakayo dumu kwa mwaka mmoja, ilikuwa muhimu kwa sababu serikali ilikuwa haijachukua hatua dhidi ya madai ya wizi wa kura uliotokea katika uchaguzi wa Novembaambapo chama cha Suu Kyi cha National League for Democracy kilipata ushindi wa kishindo.

Siku ya Ijumaa, takriban wanachama 300 wa chama cha Suu Kyi kilicho pinduliwa walitangaza kuwa ndio wawakilishi pekee halali wa wananchi na kutaka kutambuliwa ulimwenguni kuwa ndio wasimamizi wa serikali ya nchi hiyo.

Mapinduzi hayo ya kijeshi yamelaaniwa na Rais wa Marekani Joe Biden na viongozi wengine wa dunia, wakitaka serikali iliyochaguliwa na wananchi kurejeshwa madarakani.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo aghlabu hutaabika kufikia makubaliano, limetoa tamko la pamoja Alhamisi likieleza “wasiwasi mkubwa” kwa kutangazwa hali ya dharura iliyowekwa na jeshi hilo. Wanachama 15, akiwemo msimamizi wa Myanmar, China, pia imetaka kuachiwa kwa Aung San Suu Kyi, Rais Win Myint na wengine wote waliowekwa kizuizini.

FILE - Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, Feb. 26, 2020.
FILE - Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, Feb. 26, 2020.

Myanmar ikiwa ni koloni la Uingereza hadi mwaka 1948, nchi hiyo imekuwa chini ya utawala wa madikteta unaoungwa mkono na jeshi kuanzia mwaka 1962 hadi 2010.

Akiwa maarufu kati ya Wabuda waliowengi Myanmar, Suu Kyi, umri miaka 75, amejikuta umaarufu wake ukiporomoka duniani kutokana na serikali yake ilivyowatendea Waislam wa Rohingya kwa ujumla walio wachache.

Mwaka 2017, jeshi liliwanyanyasa Waislam wa Rohingya, kufuatia kushambuliwa vituo vya polisi katika jimbo la Rakhine, na kupelekea maelfu ya Waislamu wa Rohingya kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh ambapo wanaishi hadi hivi leo.

Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, inaendelea kuichunguza Myanmar kutokana na vitendo vya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

XS
SM
MD
LG