Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:33

Mawaziri wa mambo ya nje wa G7 wakemea Mapinduzi ya Myanmar


Vifaru vya jeshi la Myanmar vikifanya doria katika mji wa Mandalay baada ya jeshi la nchi hiyo kupindua serikali ya kiraia. Picha ya February 3, 2021. REUTERS/Stringer .
Vifaru vya jeshi la Myanmar vikifanya doria katika mji wa Mandalay baada ya jeshi la nchi hiyo kupindua serikali ya kiraia. Picha ya February 3, 2021. REUTERS/Stringer .

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la mataifa tajiri duniani G-7, Jumatano wamekemea mapinduzi ya nchini Myanmar.

Pia mawaziri hao wameeleza kusikitishwa kwao na kushikiliwa kwa kiongozi wa taifa hilo Aung San Suu Kyi, na viongozi wengine wa kisiasa.

Katika taarifa ya pamoja, mawaziri hao wameeleza kwamba wanapinga vikali kushikiliwa kwa viongozi wa kisiasa na wanaharakati wa asasi za kiraia, akiwemo kiongozi Aung San Suu Kyi, na rais Win Myint, na kulenga vyombo vya habari.

Wametoa wito kwa jeshi la Myanmar kumaliza kile walicho kiita hali ya dharura katika nchi na kuruhusu kutowekwa masharti kwa upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kusaidia makundi ya watu walio hatarini.

Vilevile leo hii kumeanza mgomo katika hospitali 70, na idara za afya katika miji 30 ikiwa ni hatua ya kupinga mapinduzi hayo.

XS
SM
MD
LG