Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 12:25

Serikali ya Bangladesh yakosolewa kuwahamisha wakimbizi wa Rohingya


Wakimbizi wa Rohingya wakihamishwa kwa usafiri wa meli kwenda kisiwa cha Bhasan Char, Bangladesh, Disemba 4.
Wakimbizi wa Rohingya wakihamishwa kwa usafiri wa meli kwenda kisiwa cha Bhasan Char, Bangladesh, Disemba 4.

Serikali ya Bangladesh imeanza kuhamisha kundi la pili la wakimbizi wa Kirohingya hadi kisiwa chenye hatari ya mafuriko katika ufukwe wa Bengal licha ya upinzani kutoka wanaharakati wa kutetea haki za binadamu.

Kundi la kwanza la zaidi ya Waislamu hao 1,600 kutoka Mnyanmar walisafirishwa hadi Bhasan Char mapema mwezi Disemba, na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje AK Abdulmomen amesema ni chini ya elfu moja walio katika kundi hili la pili.

Wakimbizi hao wanapelekwa katika kile anachokieleza ni kisiwa kizuri cha mapumziko.

Zaidi ya Warohingya 700,000 walikuwa wanaishi katika makambi nchini Bangladesh tangu 2017 baada ya mashambulio ya jeshi la Myanmar ambayo Umoja wa Mataifa wanasema huenda ni mauaji ya kimbari.

Baada ya kundi la kwanza kuhamishwa Disemba 4 baadhi ya Warohingya wameliambia shirika la Habari la AFP kwamba walipigwa na kulazimishwa kukubali kuhama.

Hata hivyo Umoja wa Mataifa unasema haijahusishwa kwenye utaratibu huo.

XS
SM
MD
LG