Wakati huohuo baadhi ya wahadhiri wamekataa kufanya kazi au kushirikiana na viongozi wakipinga kitendo cha jeshi kuchukua madaraka kwa nguvu.
Kampeni ya kiraia ya kutotii sheria ilianza na wafanyakazi wa afya muda mchache baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Jumatatu.
Na kuanzia wakati huo kampeni hiyo ilishika kasi na kujumuisha wanafunzi, makundi ya vijana na baadhi ya wafanyakazi katika sekta za serikali na binafsi.
Wakiwa wamevaa vitambaa vyekundu huku wakibeba mabango katika maandamano, waalimu wengi walikusanyika mbele ya majengo ya chuo kikuu cha elimu cha Yangon.
“Hatutaki mapinduzi haya ya kijeshi ambayo yalinyakua madaraka kinyume cha sheria kutoka kwa serikali yetu iliyochaguliwa”, mhadhiri New Thazin Hlaing amesema.