Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:27

Tanzania yaandaa mkakati wa ushuru wa simu za WhatsApp


Nembo ya TCRA
Nembo ya TCRA

Serikali ya tanzania inashughulikia mpango utakao iwezesha kutoza ushuru matumizi ya simu za WhatsApp ikiwa ni juhudi ya kukusanya kodi inayopoteza kutokana na kushuka kwa mapato yanayotokana na upigaji simu za kimataifa.

Kimsingi, kampuni za mawasiliano zilikuwa zinakusanya kiwango kikubwa cha mapato kila mwaka kutokana na gharama za simu za kimataifa.

Lakini tangu kutumia huduma ya WhatsApp kupiga simu, imekuwa ni njia kuu ya matumizi majumbani, kiwango kinacho kusanywa na makampuni ya simu kimeshuka kwa kiwango kikubwa kwa sababu watu wanatumia WhatsApp na aina nyingine za mawasiliano kuepuka gharama za simu za kimataifa.

WhatsApp
WhatsApp

Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kuwa idadi ya simu za kimataifa zimepungua sana katika miaka kumi iliyopita.

Kwa mfano, TCRA imerekodi jumla ya simu za kimataifa milioni 107.2 wakati wote wa robo ya nne ya mwaka 2012.

Lakini, idadi hiyo imeshuka hadi simu milioni 65 wakati wa robo ya nne ya mwaka 2016 kabla ya kupungua zaidi kufikia simu milioni 27.27 katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2020.

Lakini Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia Faustine Ndugulile, ameliambia gazete la Mwananchi katika mahojiano kuwa serikali inaangalia jinsi gani ya kuzuia hasara hii ya mapato yake, iliyosababishwa na mawasiliano ya WhatsApp.

Amesema TCRA hivi sasa inauangalia Mfumo wa Kufuatilia Njia ya Mawasiliano (TTMS), kwa mtizamo wa kupata njia bora kuzuia hasara hiyo ya mapato.

Mfumo huo uliokuwa umezinduliwa miaka miwili iliyopita, mfumo wa TTMS uliogharimu dola milioni 24.6 ulikuwa umewekwa kufuatilia simu zinazopigwa kwa wizi.

Unatumika kutambua wizi wa mawasiliano ya simu na pia miamala ya fedha ya simu na takwimu ambapo isingekuwa rahisi kupata kwa usahihi bila ya mfumo kama huo.

Mfumo huo pia unaiwezesha TCRA kuhakikisha ubora wa huduma inayotolewa na maopereta wa simu za mkononi kwa wateja wao, ameongeza.

“Tunahitaji kuwa na njia ya udhibiti na hili ndilo TCRA inafanya hivi sasa,” amesema.

Akielezea juu ya suala hilo, mkurugenzi wa masuala ya kisekta TCRA, Emanuel Manase, amesema itakuwa vigumu kwa mdhibiti wa mawasiliano kuzuia simu za WhatsApp lakini amegusia kuwa kuboresha mifumo ya udhibiti ya TCRA kutaangazia kuimarisha kipato cha serikali kwa kubuni ushuru mpya wa data.

Amesema hatua ya kwanza kufikia lengo hilo ilikuwa ni kuzitambua simu zote zinazo wasiliana kupitia mtandao wa WhatsApp na Messenger.

“Baada ya hilo, hatua ya pili itakuwa kufanya uchambuzi wa matumizi ya data ambapo tutagundua iwapo turekebishe ushuru kwa sababu kupitia njia hiyo serikali itakusanya mapato yake pamoja na kushuka kwa matumizi ya upigaji wa simu za kimataifa,” amesema.

Hilo likisha fanyika, amesema, serikali baada ya hapo itaamua hatua itakayo chukua.

XS
SM
MD
LG