Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:01

Tanzania yafafanua sharti la leseni kwa vyombo vya habari vya kimataifa


Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania
Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania

Serikali ya Tanzania imetolea ufafanuzi hatua yake ya kuvitaka vyombo vya habari vya Kimataifa kupata kwanza leseni kutoka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA .

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi amesema lengo la kutaka vyombo va nje vinavyo tangaza na vyombo vya habari vya hapa nchini kupata kwanza leseni ni kutaka kutambua vyombo hivyo vinashirikiana na vyombo gani vya hapa nchini na sio kuvizuia kutangaza na kuendesha vipindi vyake kama inavyoripotiwa.

Waziri Kabudi ametoa ufafanuzi huo katika mazungumzo yake aliyoyafanya jijini Dar es Salaam na Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini David Concar na kufafanua kuwa mpaka sasa vyombo vyote vya habari vya Kimataifa vimekwishatekeleza matakwa hayo ya kisheria na kupata leseni ya kutangaza na kuendesha vipindi vyao

Kuhusu suala la mabadiliko ya sheria za asasi za kiraia (NGOs) na vyama vya siasa Waziri amesema kuwa lengo lake lilikuwa ni kuongeza uwazi na uwajibikaji katika fedha zinazoingia kwa asasi hizo pamoja na matumizi yake na kuwa linaendana na sheria na taratibu za kimataifa za kuzuia utakatishaji wa fedha

Balozi Concar pamoja na kuzungumzia masuala mengine ya kidiplomasia na maendeleo alilenga kuangalia namna ya kuondoa malalamiko kutoka kwa baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na vyombo vya habari vya kimataifa juu ya matakwa hayo mapya ya kisheria.

XS
SM
MD
LG