Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:07

Ajali ya moto yauwa wanafunzi 10 Tanzania


Ramani ya Tanzania
Ramani ya Tanzania

Wanafunzi 10 wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa vibaya baada ya shule ya msingi Byamungu Islamic Mkoani Kagera kuungua kwa moto usiku wa kuamkia Jumatatu.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa umri wa wanafunzi waliofariki katika shule hiyo iliyoko kata ya Itera wilayani Kyerwa ni kati ya miaka sita hadi 12.

Habari zaidi zinaeleza kuwa wanafunzi sita waliojeruhiwa wamepelekwa katika Hospitali ya Nyakahanga wilayani Karagwe huku mmoja amepelekwa katika hospitali ya Nkwenda kwa matibabu zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Marco Gaguti na kamati yake ya ulinzi na usalama wamefika katika eneo la tukio na kusema kuwa serikali imeunda tume ya kuchunguza chanzo cha moto huo na kwamba imefungwa kwa muda wa wiki mbili kuanzia sasa.

Naye Mganga Mkuu wa hospitali ya nyakahanga Dkt Furaha Kahindo amesema kuwa baadhi ya majeruhi wanaendelea vizuri.

Wakati huohuo baadhi ya wazazi na mashuhuda wameitaka serikali kufanya uchunguzi zaidi juu ajali hiyo kwenye shule hiyo yenye wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la sita.

XS
SM
MD
LG