Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:20

Jaji mstaafu Mark Bomani aaga Dunia


Marehemu Jaji Paul Bomani
Marehemu Jaji Paul Bomani

Jaji mstaafu wa Tanzania Mark Bomani amefariki dunia usiku wa kuamkia Ijumaa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Bomani alikuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza nchini.

Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, amethibitisha kifo cha Bomani ambaye alilazwa hospitalini hapo kwa siku 24.

“Jaji Mstaafu amefia hapa Muhimbili, amefariki majira ya saa 4:00 usiku wa kuamkia Ijumaa, na alikuwa hapa hospitalini kwa siku 24,” ameeleza Aligaesha.

Wakati huohuo Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole ameandika kupitia Twitter : “Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa huzuni taarifa ya kifo cha Jaji (Mst) Mark Bomani, MwanaCCM & Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Tanzania, Uongozi unatoa pole kwa familia, wafiwa & wote walioguswa na msiba huu. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe”

XS
SM
MD
LG