Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:06

Vienna : Wanadiplomasia warejea kujadili suala la nyuklia la Iran


Balozi wa kudumu wa China Umoja wa Mataifa Wang Qun, akizungumza na waandishi wa habari wakati kikao cha JCPOA cha Tume ya Pamoja kikiendelea huko Vienna, Austria, Aprili 27, 2021.
Balozi wa kudumu wa China Umoja wa Mataifa Wang Qun, akizungumza na waandishi wa habari wakati kikao cha JCPOA cha Tume ya Pamoja kikiendelea huko Vienna, Austria, Aprili 27, 2021.

Pande husika katika makubaliano ya nyuklia ya Iran zitaanza mashauriano ya raundi ya tatu huko Vienna yenye lengo la kuirudisha Marekani kushiriki katika mkataba huo.

Mkataba huo, unaozuia progamu ya nyuklia ya Iran kwa mabadilishano ya unafuu wa vikwazo, ulikuwa uko mahututi tangu pale Rais Donald Trump alipoiondoa mwaka 2018.

Washirika waliobakia kwenye mkataba wa 2015 wameendelea kujihusisha katika mashauriano tangu mapema Aprili kujaribu kuufufua tena.

Raundi ya tatu ya mazungumzo ilianza Jumanne na baada ya siku kadhaa za majadiliano ya kiufundi kati ya kikundi cha wataalam na wajumbe, yataanza tena Jumamosi.

Josep Borrell
Josep Borrell



Mkuu wa huduma za sera za mambo ya nje katika EU Josep Borrell amesema katika taarifa yake kuwa wajumbe kutoka Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani, Iran na Russia watakutana ana kwa ana majira ya saa tisa mchana (1300 GMT).

“Washiriki wataendelea na majadiliano kwa uwezekano wa Marekani kurejea katika JCPOA na jinsi ya kuhakikisha utelekezaji kamili na ufanisi wa JCPOA,” taarifa hiyo imeeleza, ikutumia herufi za mkato za jina ya makubaliano hayo rasmi.

Baada ya mazungumzo, wajumbe watarejea katika miji mikuu yao kupokea maelekezo, wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema.

Mwanadiplomasia mmoja wa Ulaya amesema wajumbe kutoka Marekani, Ulaya, Russia na China walifanya mkutano wa pamoja Jumamosi asubuhi, lakini bila ya mwakilishi kutoka Iran wakati Tehran ilikataa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani.

Pamoja na kujiondoa katika muafaka huo, utawala wa Trump uliweka vikwazo vya jumla dhidi ya Iran, na yenyewe ilianza kuongeza harakati zazke za nyuklia.

Rais mpya wa Marekani Joe Biden anaunga mkono mkataba huo – ambao Iran iliendelea kuutekeleza kabla ya vikwazo vya Trump – lakini ameitaka Tehran kusitisha hatua ilizochukua kuhusu nyuklia kabla Washington haijasitisha vikwazo dhidi yao.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Baada ya kipindi cha takriban mwezi mmoja wa mazungumzo, pande hizo husika wiki hii zilieleza nia ya “kuharakisha” mazungumzo hayo.

Matumaini ya mazungumzo hayo ni kufikia matokea ya msingi “ ifikapo mwisho wa mwezi Mei” – kabla ya uchaguzi wa rais Iran – mwanadiplomasia ambaye ana uzoefu na mazungumzo hayo ameliambia shirika la habari la AFP wakati wa raundi ya mwisho ya mazungumzo.

XS
SM
MD
LG