Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:44

Marekani na Iran wakubali kukutana katika duru ya pili

Afisa wa siasa wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, kulia, akiwasili katika Hoteli ya Grand Wien kuhudhuria mazungumzo ya nyuklia yanayo fanyika, Vienna, Austria, Jumanne, April 6, 2021. (AP Photo/Florian Schroetter)

Marekani na Iran wamekubaliana kwa duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja huko Vienna wiki ijayo.

Mazungumzo hayo ni kwa lengo la kujaribu kila mmoja kurejea katika utekelezaji wa mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015.

Lakini Iran imesisitiza kwamba vikwazo vyote vya Marekani dhidi yake viondolewe na Marekani imeonya kwamba dai kama hilo huenda likapelekea mvutano.

Afisa mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ambaye alizungumza na wanahabari Ijumaa amesema kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja huenda yakaanza tena katikati ya wiki ijayo katika mji mkuu wa Austria.

Wanadiplomasia wa Marekani na Iran wamehitimisha duru ya awali ya mikutano mapema Ijumaa, huku wapatanishi wa Umoja wa Ulaya wakitoa ujumbe kati ya pande hizo mbili.

XS
SM
MD
LG