Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:20

Marekani yawataka waasi wa Kihouthi kuepusha mashambulizi mapya


Msemaji wa Mambo ya Nje Ned Price(Nicholas Kamm/Pool via AP)
Msemaji wa Mambo ya Nje Ned Price(Nicholas Kamm/Pool via AP)

Marekani inatoa wito kwa waasi wa Kihouthi nchini Yemen kuepuka mashambulizi mapya ya kijeshi ndani ya Yemen, na kusitisha mashambulio yanayoathiri maeneo ya raia nchini Saudi Arabia.

Katika taarifa yao Jumapili jioni msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ned Price alisema Marekani inasikitishwa sana kuendelea kwa mashambulio ya Wahouthi.

Amesema tunawasihi Wahouthi wajiepushe na vitendo vya kudhoofisha na kuonyesha nia yao ya dhati kushiriki vyema katika juhudi za Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths kutafuta amani, alisema Price. Wakati ni sasa wa kumaliza mzozo huu.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Griffiths alianza mazungumzo ya siku mbili nchini Iran Jumapili wakati akishinikiza kupatikana kwa mashauriano ya kisiasa kwa mzozo wa Yemen, ambao ulianza mwishoni mwa mwaka 2014 kwa Wahouthi kuuteka mji mkuu wa nchi hiyo.

Saudi Arabia ilianzisha kampeni ya kijeshi kuitetea serikali inayotambuliwa kimataifa ya Yemen mapema mwaka 2015.

XS
SM
MD
LG