Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:53

Rais Biden aahidi kuendeleza diplomasia ya Marekani Ulimwenguni


Rais Joe Biden akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje Feb. 4, 2021, in Washington.
Rais Joe Biden akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje Feb. 4, 2021, in Washington.

Rais mpya wa Marekani ameweka dhahiri kuwa ulimwengu utarajie Marekani yenye diplomasia zaidi kuelekea mbele akianza kwa kusitisha mpango wa rais aliyeondoka Donald Trump wa kuondoa maelfu ya wanajeshi wa Marekani walioko Ujerumani.

Biden ameyasema hayo Alhamisi jioni akiwa kwenye wizara ya mambo ya nje ambapo aliambia wafanyakazi pamoja na wanadiplomasia kuwa wao ndiyo sura ya Marekani, na kwamba sasa Marekani imerejea tena kwenye nafasi yake.

Miongoni mwa mengine aliyosema ni kipaumbele chake ni mapinduzi ya Burma, mazungumzo na Russia pamoja na uhusiano na China.

Wakati akisisitiza mtazamo mpya kwenye sera za kigeni, rais Joe Biden amesema kuwa atasitisha kurejeshwa kwa wanajeshi wa Marekani walioko Ujerumani pamoja na kusitisha uungaji mkono wa Saudi Arabia kwenye mapigano ya Yemen.

Hatua nyingi za utawala mpya wa Biden zinaashiria nia yake kwa ulimwengu kuwa Marekani imechukua tena nafasi yake baada ya miaka minne ya utawala wa Trump uliokuwa na kauli mbiu ya Marekani kwanza. Biden wakati wa hafla hiyo alikuwa ameandamana na makamu wake wa Rais Kamala Harris.

Rais Biden anaeleza : "Marekani imerejea tena, Marekani imerejea tena. Diplomasia imerejeshwa. Ninyi ni kutovu na moyo wa malengo yangu. Tutaimarisha tena ushirikiano wetu. Tutashauriana tena na dunia pamoja na kukabiliana na matatizo yalioko mbele yetu kama janga la corona, mabadilko ya hali ya hewa pamoja na kuzingatia democrasia na haki za kibinadamu kote ulimwenguni."

Biden amesema kuwa katika siku chache zilizopita, wamekuwa wakishauriana na washirika wao ili kuleta pamoja jamii ya kimataifa ili kushugulikia swala la mapinduzi ya Burma.

Rais wa Marekani alisema : "Tumekubaliana kwa hilo kwamba hakuna demokrasia inayopinga uamuzi wa watu wake na kupuuza matokeo ya uchaguzi. Ni sharti jeshi la Burma lirejeshe madaraka pamoja na kuachilia huru wanaharakati na maafisa waliozuiliwa. Vile vile ni lazima lifungulie mawasiliano pamoja na kujiepusha na ghasia."

Biden ameongeza kusema kuwa Marekani itakabiliana na China kutokana na ukatili wa kiuchumi pamoja na kuchukua tena nafasi yake kwenye taasisi za kimataifa ambayo imepotea kwa muda mrefu.//

Biden amesema : "Tutakabiliana na ukatili wa kiuchumi wa China pamoja na kudhibiti ukiukaji wake wa haki za binadamu, haki za ubunifu na utalawa wa dunia. Hata hivyo tuko tayari kushauriana na China iwapo hilo litatunufaisha."

Biden pia amesema kuwa Marekani itasitisha uungaji mkono wa Saudi Arabia kwenye mapigano ya Yemen yaliyo chukua muda mrefu akisema kuwa lazima yakomeshwe ili kufikisha kikomo moja wapo ya majanga makubwa zaidi ya kibinadanu ulimwenguni.

Ameongeza kusema kuwa Marekani itaongeza idadi ya wakimbizi wanaoruhusiwa kuingia hapa Marekani kwa zaidi ya mara nane ya pale utawala wa Trump ulipoachia.

Hatua ya Biden itaongeza idadi hiyo hadi 125,000 kupita ile iliyowekwa na rais Barack Obama wakati akiondoka ofisini ya 15,000. Trump kabla ya kuondoka ofisini alipunguza idadi hiyo tena hadi 15,000. Biden pia aliweka dhahiri kwa Rais wa Russia Vladimir Putin kwamba siku za kuchezea Marekani zimekwisha.

Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Ziara ya Biden Alhamisi kwenye ofisi za wizara ya mambo ya nje imekuja baada ya hatua yake ya Jumatano ya kuongeza muda wa mkataba unaodhibiti viwango vya umiliki wa silaha za nyuklia ikiwa imebaki siku mbili tu kabla ya kimalizika.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Harrison Kamau, VOA Washington DC.

XS
SM
MD
LG