Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:59

Rais Biden asaini amri za kiutendaji kuunga mkono haki za kijamii


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Mwaka wa mwisho wa utawala wa Rais wa zamani Donald Trump ulishuhudia wimbi kubwa la maandamano na malalamiko ya kulaani ukatili unaofanywa na polisi na kudai haki sawa za kijamii.

Lakini kufikia mwisho wa mwaka 2020 nguvu za vuguvugu la Black Lives Matter lililoongoza maandamano hayo zilipunguwa na hoja kutolewa nini kinacho hitajika kufanyika kufikia malengo yao.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Esha Sarai amezungumza na wanaharakati, na walio tayarisha maandamano na malalamiko kote nchini na kuwauliza juu ya mustakbali wa vuguvugu lao chini ya utawala wa Rais Joe Biden na wademokrats wakishikilia madaraka.

Hivyo basi wiki moja tu baada ya Rais Joe Biden kuingia madarakani tayari amesaini amri kadhaa za kiutendaji kuunga mkono haki za kijamii , baada ya miezi kadhaa ya maandamano kuunga mkono vuguvugu la Black Lives Matter.

Description: FILE - Nov. 7, 2020, Watu walikusanyika katika mtaa wa Black Lives Matter Plaza kusheherekea ushindi wa Rais mteule Joe Biden kuwa rais wa 46th wa Marekani. (AP Photo/Alex Brandon, File)
Description: FILE - Nov. 7, 2020, Watu walikusanyika katika mtaa wa Black Lives Matter Plaza kusheherekea ushindi wa Rais mteule Joe Biden kuwa rais wa 46th wa Marekani. (AP Photo/Alex Brandon, File)

Biden ameeleza : "Wakati wa kampeni yangu kugombania kiti cha rais , nilieleza bayana kwamba muda muafaka umefika kwa taifa kuchukua hatua. Tumekuwa na mgawanyiko mkubwa wa ukosefu wa haki za kijami na rangi katika mfumo wa maisha ya Marekani, mfumo wa ubaguzi ulioathiri taifa hili kwa muda mrefu sana."

Lakini baadhi ya wanaharakati hawaamini rais ataweza kutekeleza kikamilifu matakwa ya vuguvugu lao kama vile kuchukua sehemu ya fedha zinazo gharimia vikosi vya polisi na kutumia kwa mambo mengine, na kupiga marufuku jela za serikali kuu zinazo endeshwa na watu binafsi, ingawa Biden alisaini amri wiki hii ya kufutilia mbali kandarasi za jela zinazo endeshwa na watu binafsi kwa awamu.

Reese Monson muandamanaji mjini Portland anasema hawajafurahia sana kuchaguliwa kwake.

Monson anaeleza kuwa : "Hatuja hamasishwa sana naye, lakini tuna matumaini ataleta mabadilko mengi na kuwafanyia watu wetu mambo mazuri. Lakini hakua ni chagua letu la kwanza lakini vile vile alikuwa chaguo pekee. Ni afadhali kuwa naye kuliko Donald Trump.

Baadhi ya wana harakati wanasema jambo kubwa ni kumshinikiza Biden kuimarisha kazi zinazo fanywa mashinani katika jamii mbali mbali ya watu weusi waliomsaidia kupata ushindi.

Aaron Rogers, mwanaharakati mjini St Louis anasema : "Muda mfupi tu kabla ya kuwa rais tulishuhudia shinikizo kubwa kuwahi kushuhudiwa kutoka makundi ya mashinani, watu wa mitaani kote nchini, hasa wanao husiana na Black Lives Matter, wakitaka megeuzi ya dhati ya usawa wa kijamii na haki yafanyike."

Ingawa baadhi ya maandamano dhidi ya ukosefu wa haki za kijamii yamekumbwa na ghasia ambazo zimelaaniwa na wote Trump na Biden, lakini kwa sehemu kubwa vuguvugu limekuwa likitetea maandamano ya amani na kuhimiza umuhimu wa kufanya kazi katika ngazi zote za kijamii.

Rais wa zamani Donald Trump na Rais Joe Biden aliyeshinda uchaguzi wa urais.
Rais wa zamani Donald Trump na Rais Joe Biden aliyeshinda uchaguzi wa urais.

Jilisa Milton muasisi wa BLM mjini Mirmingham, anasema mambo mengi yanafanyika katika miji na vijiji ingawa hayagongi vichwa vya habari kwa lengo la kuendelea na mjadala wa kutaka mageuzi.

Wana harakati wana matumaini majadliano yataendelea kuwa na umuhimu mjini Washington vile vile.

XS
SM
MD
LG