Mkutano huo umehamishwa kutoka makao yake ya kawaida mjini Davos Uswiss na kupelekwa Singapore kutokana na wasiwasi wa kusambaa kwa janga la covid 19 barani Ulaya.
“Kiasili Singapore imekuwa na uhusiano wa karibu sana na Marekani lakini pia inashirikiana vizuri na China,” Borge Brende amesema katika majadiliano kwa njia ya mtandao na Waziri Mkuu wa Singapore, Lee Hsien Loong.
“Pengine katika mkutano wa Singapore ambao utakuwa mkutano maalum wa mwaka, huenda itakuwa mahali ambapo utaona utawala mpya wa Biden na ule wa China wakikutana,” ameongeza.
Si China wala Marekani zimesema kama zitatuma maafisa wake kwenye mkutano wa Singapore, ambapo bado hakuna uhakika wa kufanyika mkutano kwa sababu ya janga la Corona ambalo linazidi kuongezeka katika sehemu nyingi za dunia.