Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:16

Timu ya WHO yaanza kuchunguza asili ya janga la Corona China


Timu ya wataalam kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni -WHO ilipelekwa China kuchunguza asili ya janga la COVID-19 wakipanda basi kabla ya kuondoka uwanja wa ndege wa Wuhan Tianhe, Wuhan, jimbo la Hubei,
China Januari 14, 2021.REUTERS/Thomas Peter
Timu ya wataalam kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni -WHO ilipelekwa China kuchunguza asili ya janga la COVID-19 wakipanda basi kabla ya kuondoka uwanja wa ndege wa Wuhan Tianhe, Wuhan, jimbo la Hubei, China Januari 14, 2021.REUTERS/Thomas Peter

Timu ya wataalam kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni -WHO iliwasili katikati ya jiji la China la Wuhan Alhamisi kuchunguza asili ya janga la COVID-19.

Timu hiyo ya kimataifa yenye watu 10 iliruka kwenda Wuhan baada ya kuchukua ndege ya moja kwa moja kutoka Singapore.

Baada ya kuwasili timu hiyo mara moja ikaingia katika kipindi cha siku 14 za kujitenga.

Wanachama wengine wawili wa timu ya WHO walibaki Singapore baada ya kupimwa na kukutwa na virusi vya Corona.

Taarifa hiii ni kulingana na mfuatano wa ujumbe kadhaa kwa njia ya tweeter kutoka kwenye shirika hilo.

Virusi hivyo vilipatikana kwa mara ya kwanza huko Wuhan mwishoni mwa mwaka 2019.

Hatimaye virusi hivyo vikaenea karibu katika kila kona ya ulimwengu, na kusababisha zaidi ya vifo milioni 1.9 kati ya zaidi ya milioni 92.3 ya maambukizi, kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani.

XS
SM
MD
LG