Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:15

Mwandishi aliyetoa habari za kwanza kabisa kuhusu Corona ahukumiwa China


C
C

Mwandishi wa habari, Raia wa China ambaye amekuwa akizuiliwa gerezani tangu mwezi wa tano kwa kuonyesha moja kwa moja kupitia mtandao wa kijamii, mlipuko wa virusi vya Corona katika mji wa Wuhan, amehukumiwa kifungo cha miaka 4 gerezani.

Hukumu yake imekuja mwaka mmoja baada ya mlipuko wa virusi hivyo ambavyo mwanzoni vilikuwa vinatajwa kuwa homa ya mapafu.

Zhang Zhan, ambaye alikuwa wakili, ameshutumiwa kwa kile kimetajwa kama kuanzisha ugomvi na kusababisha shida, kwa kuripoti kuhusu virusi hivyo wakati vilipolipuka mjini Wuhan.

Ripoti zake za moja kwa moja za video na maandishi, zilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii mwezi Februari.

Maafisa nchini China wamewaadhibu watu kadhaa waliotoa habari kuhusu kuwepo kwa virusi hivyo, katika hatua ya kunyamazisha wakosoaji wa serikali namna ilivyoshughulikia mlipuko wa virusi vya Corona.

Beijing imejisifu sana kwa kile imetaja kama kufanya kazi kubwa kupata mafanikio makubwa katika kukabiliana na virusi vya Corona ndani ya mipaka yake.

Imesema kwamba uchumi wake umeanza kukua.

Nchi zingine zinapitia wakati mgumu sana kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

China imechukua katua kali kuzuia usambasaji wa habari kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.

XS
SM
MD
LG