Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:30

China yaidhinisha matumizi ya chanjo yenye ufanisi wa asilimia 79.3


Wasimamizi wa sekta ya afya nchini China wamesema kwamba wameidhinisha chanjo dhidi ya virusi vya Corona ambayo imetengenezwa na kampuni inayomilikiwa na serikali ya Sinopharm.

Naibu wa kamisaa wa tume ya usimamizi wa dawa nchini China Chen Shifei, ameambia waandishi wa habari mjini Beijing kwamba hatua hiyo imefanyika jana usiku.

Chanjo hiyo ya dozi mbili ni ya kwanza kuidhinishwa kwa matumizi ya kawaida nchini China.

Hatua hiyo inajiri wakati nchi hiyo inaendelea kufanya kampeni ya kutoa chanjo kwa watu milioni 50 kabla ya maadimisho ya mwaka mpya nchini China, unaoadhimishwa mwezi Febrauri.

Chanjo hiyo imetengenezwa na taasisi ya biolojia ya Beijing, ambayo sehemu yake inamilikuwa na kampuni ya Sinopharm.

Kampuni hiyo imesema kwamba utafiti wa awali unaonesha kwamba chanjo yake ina ufanisi wa asilimia 79.3.

Kampuni ya Sinopharm ni mojawapo ya kampuni za kutengeneza dawa nchini China, ambazo zinatengeneza chanjo dhidi ya virusi vya Corona, ambavyo vimeua zaidi ya watu milioni 1.8 kote duniani.

XS
SM
MD
LG