Awali, China ilipinga wito wa uchunguzi wa kimataifa kuhusu kiini cha virusi vya corona, ikisema wito huo ni dhidi ya China, lakini ilikuwa wazi kwa uchunguzi utakao ongozwa na WHO.
Lakini haijawa wazi iwapo wachunguzi hao wa WHO watasafiri kwenda mji wa Wuhan ambao ndio ulikuwa kitovu cha virusi vya corona, na mazungumzo yanaendelea kuhusu safari hiyo.
“WHO inaendelea kuwasiliana na china na kujadili juu ya timu ya kimataifa na mahali timu hiyo itatembelea”. Babatunde Olowokure, mkurungezi wa WHO anayehusika na dharura za kikanda magharibi mwa Pacific, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari Alhamisi.
Jumatano, afisa wa WHO na wanadiplomasia waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba tume ya WHO inatarajiwa kwenda China wiki ya kwanza ya mwezi Januari, kuchunguza kiini cha virusi vya corona.