Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:57

Rais Xi ampongeza Rais mteule wa Marekani Joe Biden


FILE - Mwezi Desemba. 4, 2013, Rais Xi Jinping, kulia, akiwa na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden katika ukumbi wa Great Hall of the People mjini Beijing.
FILE - Mwezi Desemba. 4, 2013, Rais Xi Jinping, kulia, akiwa na Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden katika ukumbi wa Great Hall of the People mjini Beijing.

Rais wa China Xi Jinping amempongeza rais mteule wa Marekani Joe Biden.

Kupitia ujumbe wa telegram, Xi amesema mataifa yote mawili sasa yanahitaji kuzingatia ushirikiano usio na migogoro ili kuimarisha amani na maendeleo kote ulimwenguni, Shirika la habari la serikali ya China Jumatano limeripoti.

Ujumbe wa kiongozi huyo wa China umekuja wiki mbili baada ya viongozi wengine wa ulimwengu kumpongeza Biden.

Uhusiano wa Marekani na China umeshuka kwa kiwango kikubwa katika miezi ya karibuni wakati kukiwa na migogoro ya kibiashara na kiteknolojia pamoja na lawama za ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa habari.

Mataifa yote mawili pia yamelaumiana kuhusiana na yalivyo chukulia janga la virusi vya corona wakati Washington ikidai kuwa China ilichukuwa muda mrefu kuufahamisha ulimwengu kuhusu kuzuka kwa virusi hivyo mjini Wuhan.

Makamu wa rais wa China Wang Qishan pia ametuma ujumbe wa pongezi kwa Biden taarifa zimeongeza.

XS
SM
MD
LG