Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:21

Wanasayansi wa WHO kwenda Wuhan kuchunguza asili ya janga la Corona


Mwanasayansi mkuu wa WHO Soumya Swaminathan akizungumza na wanahabari huko Geneva, July 3, 2020.(Reuters).
Mwanasayansi mkuu wa WHO Soumya Swaminathan akizungumza na wanahabari huko Geneva, July 3, 2020.(Reuters).

China inasema timu ya wanasayansi kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni itawasili wiki hii huko Wuhan kuanza uchunguzi wake wa asili ya janga la virusi vya corona.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje Zhao Lijian alisema Jumanne kwamba timu hiyo ya washiriki 10 itaondoka kutoka Singapore Alhamisi hii na kuruka moja kwa moja kuelekea Wuhan, jiji la kati ambalo virusi vya corona iligunduliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa 2019.

Hatimaye virusi vilienea karibu kila kona ya ulimwengu, na kusababisha vifo vya zaidi ya milioni 1.9 kati ya karibu maambukizo milioni 91.

China imetaka kubadilisha hadithi juu ya asili ya virusi, huku maafisa wakishinikiza nadharia ugonjwa uliibuka kwanza katika taifa jingine.

Daktari Mike Ryan, mkuu wa mpango wa dharura wa WHO, aliwaambia waandishi wa habari huko Geneva Jumatatu kwamba shirika hilo "linatafuta majibu hapa ambayo yanaweza kutuokoa katika siku zijazo. Sio wakosaji na wala sio watu wa kulaumiwa.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG