Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:16

Shambulizi Hodeidah lauwa 10, Waziri awalaumu wapiganaji wa Kihouthi


Ramani ya Yemen ikionyesha eneo la Hodeidah lililoshambuliwa na mizinga.
Ramani ya Yemen ikionyesha eneo la Hodeidah lililoshambuliwa na mizinga.

Karibu watu wanane wameuawa kutokana na mashambulizi ya mizinga kwenye uwanja wa kiwanda kimoja katika mji muhimu wa kijeshi, Hodeidah nchini Yemen.

Waziri wa Habari wa Yemen Moammae al Eryani amewalaumu wapiganaji wa Kihouthi kwa shambulio hilo aliloliita ni la kigaidi lililotokea Alhamisi kwenye kiwanda cha Thabit Brothers.

Wafanyakazi wa afya nchini Yemen wanasema kuna watu 10 ndio waliofariki na waziri amesema kuna wafanyakzi wengine 13 waliojeruhiwa.

Mapigano yameongezeka katika mji huo muhimu wa kuwaslisha misaada wa dharura kwa Yemen ambako makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa kati ya serikali inayoungwa mkono na muungano wa nchi za Kiarabu na wapiganaji wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa muafaka huo ulitokana na upatanishi wa Umoja wa Mataifa ambao umekuwa kwa sehemu kubwa ukiheshimiwa.

XS
SM
MD
LG