Shirika la umoja wa mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) linasema maisha ya ma elfu ya Watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano nchini Yemen, yamo hatarini kutokana na hali ya utapiamlo mbaya sana.
Taarifa iliotolewa na UNICEF jana inasema hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya kusini mwa taifa hilo, ambapo nusu millioni ya visa vya utapia mlo vimeripotiwa, huku mtoto mmoja kati ya watano akisumbuliwa na utapiamlo mbaya.
Uchunguzi wa UNICEF unaonyesha kuwa visa vya utapiamlo wa kawaida vimeongezeka kwa asilimia 10, na visa vya utapiamlo mbaya vimeongezeka kwa asilimia 15.5 mwaka huu.
Ripoti ya UNICEF inasema Watoto elfu 98 wako katika hatari ya kupoteza maisha iwapo hawatapata msaada wa dharura.
Taarifa hiyo ya UNICEF inasema, kando ya Watoto, robo millioni ya akinamama wajawazito au wanaonyonyesha wanahitaji huduma dhidi ya utapiamlo.
Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC