Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:43

Marekani, UN zapongeza makubaliano ya amani yaliofikiwa Yemen


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Viongozi wa dunia wamepongeza makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya serikali ya Yemen na wapiganaji wanaotaka kujitenga wa Yemen Kusini wa kundi la Southern Transitional Council, STC.

Rais Trump ameandika ujumbe wa Tweeter akisema ni mwanzo mwema na mwana mfalme mrithi wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman aliyeongoza juhudi za mazungumzo hayo ya Riadh anasema makubaliano ni kipindi kipya cha utulivu kwa Yemen.

Kwa upande wake mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya Yemen Martin Griffiths amesema makubaliano ya Riadha yatahamasisha juhudi za kufikia makubaliano katika hatua ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Yemen vilivyo haribu kabisa taifa hilo.

Chini ya makubaliano hayo serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa na kuongozwa na Abd Rabbo Mansour itarudi katika mji mkuu wa muda wa Aden katika muda wa siku saba zijazo.

Vikosi vyote vya kijeshi na usalama vitakuwa chini ya wizara ya mambo ya ndani ikishirikiana na ile ya ulinzi.

Serikali mpya ya Yemen itaundwa ikiwa na wajumbe sawa kutoka majimbo ya kaskazini na kusini.

Rais Trump kwenye ujumbe wake amesema makubaliano hayo ni hatua muhmu kwa nchi hiyo kuelekea mbele katika kuunda Yemen mpya iliyoungana.

XS
SM
MD
LG