Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:07

UN : Raia 17 wauawa katika shambulizi la tatu soko la Yemen


Mtoto aliyeathirika na utapiamlo kutokana na vita vinavyoendelea nchini Yemen.
Mtoto aliyeathirika na utapiamlo kutokana na vita vinavyoendelea nchini Yemen.

Raia kumi na saba wameuawa katika shambulizi lililofanyika katika soko lilioko mkoa wa Saada ulioko magharibi ya Yemen, Umoja wa Mataifa (UN), imesema, ikiwa ni shambulizi la mauaji la tatu katika eneo hilo hilo katika kipindi cha mwezi mmoja.

Mashambulizi hayo yamekuja hata baada ya kuwepo utulivu wa hali fulani nchini Yemen, ambapo mapigano makubwa kati ya majeshi ya serikali – yanayoungwa mkono na ushirika wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia – na waasi wa Kihuthi wenye mafungamano na Iran kusitisha uhasama kwa kiwango kikubwa.

UN imesema wahamiaji kutoka Ethiopia ni kati ya raia 17 waliouawa katika tukio hilo Jumanne katika soko la Al-Raqw katika mkoa wa Saada, ambao ni ngome ya Wahuthi.

Watu wasiopungua 12 walijeruhiwa, imesema, bila ya kutaja nani alihusika au silaha gani ilitumika.

Ushirika unaoongozwa na Saudi umekiri kuwa siku ya Alhamisi ulifanya mashambulizi katika mji wa Monabbih, wilaya ya Saada ambako soko hilo liko.

Novemba 22 shambulizi katika soko la Al-Raqw liliuwa raia 10, wakiwemo raia wa Ethiopia, na baada ya siku chache baadae, raia wasiopungua 10 waliuawa na wengine 22 kujeruhiwa katika tukio hilo la pili.

UN inasema raia 89 ima wameuawa au kujeruhiwa katika mashambuliz katika soko hilo la Al-Raqw.

Maelfu ya watu, wengi wao raia, wameuawa na mamilioni kulazimika kuhama makazi yao tangu Machi 2015, wakati ushirika wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia kuingilia kati vita vya Yemen.

XS
SM
MD
LG