Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:08

Wahamiaji 3,500 kutoka Afrika washikiliwa Yemen


Wahamiaji haramu wa Afrika wakiwa ndani ya boti upande wa Kusini wa bandari ya mji wa Aden 26, 2016, kabla ya kurudishwa makwao.
Wahamiaji haramu wa Afrika wakiwa ndani ya boti upande wa Kusini wa bandari ya mji wa Aden 26, 2016, kabla ya kurudishwa makwao.

Maafisa wa usalama wa Yemen wanawashikilia wahamiaji zaidi ya 3,500 kutoka Afrika walioingia nchini humo kinyume cha sheria huku mipango ikiendelea kuwarudisha katika nchi zao.

Wahamiaji hao ambao wengi wao wamekimbia vita na umasikini katika nchi zao, wanashikiliwa kwa muda katika uwanja wa mpira wa miguu katika mji wa Aden ulioko kusini mwa Yemen.

wamekuwa wakipatiwa chakula na maji na mashirika ya misaada ya Emirati Red Crescent na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia uhamiaji IOM.

Yemen ni njia ya wahamiaji wengi kutoka Afrika kuelekea katika nchi tajiri za Kiarabu ambako wanakwenda kutafuta maisha bora.

"Hii yote ni kwa sababu tunataka kusafiri. Hatutaki kukaa Yemen,Yemen ilikuwa ni njia tu. Tulianza safari siku ambayo hakukuwa na mapigano na tukachukua route ya Yemen mpaka Saudi. Lakini sasa Yemen ina matatizo mengi, watu wanauawa na risasi kila sehemu," amesema Ahmed Salman - Mhamiaji kutoka Ethiopia.

Idadi kubwa ya wahamiaji waliokamatwa wanatoka Ethiopia na Eritrea ambazo zinaaminika kuwa na asilimia 92 ya wahamiaji wote wanaoingia Yemen kutoka Afrika kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2018 ya shirika linaloshughulikia uhamiaji duniani IOM.

Mfanyakazi wa IOM Olivia Headon anasema msaada unahitajika kwa wahamiaji hao. Anaeleza : "Tuko hapa katika uwanja wa mpira mjini Aden ambapo maelfu ya wahamiaji wameletwa. Hali ni mbaya kwahivyo tunafanya kazi na washirika wetu wa umoja wa mataifa na mashirika mengine kuona tunavyoweza kusaidia huduma muhimu. Hapa sio suluhisho la kudumu. Chochote kitakachotokea ikiwa watapelekwa sehemu nyingine ama kupewa msaada wa aina fulani, lazima hayo yafanyike kwa ubinadamu."

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG