Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:57

Tanzania yashikilia wahamiaji 72 kutoka Ethiopia


Ramani iliotolewa na jumuiya ya wahamiaji ikionyesha wanaoshiriki mafunzo yanayotolewa na nchi zao, wengi wanatokea Ethiopia.
Ramani iliotolewa na jumuiya ya wahamiaji ikionyesha wanaoshiriki mafunzo yanayotolewa na nchi zao, wengi wanatokea Ethiopia.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani inawashikilia wahamiaji haramu 72 kutoka Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila ya kibali wakiwa safarini kwenda Afrika ya Kusini.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Tanzania wahamiaji hao walikamatwa Jumamosi saa 3:30 asubuhi kwenye Pori la Ranchi ya Taifa (NARCO) Kata ya Vigwaza, Chalinze wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

“Mbali ya wahamiaji hao haramu, pia tunamshikilia Rajabu Hitaji (30) mkazi na mfanyabiashara wa eneo hilo baada ya msako mkali uliofanywa na makachero wa Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Jonathan Shana alisema baada ya kupata taarifa kuwa kuna wahamiaji haramu wameingia bila ya kibali walichukuwa hatua.

Alisema wahamiaji hao haramu baada ya kugundua kuwa kuna gari la polisi linawafuatilia, waliingia kwenye hifadhi hiyo kwa lengo la kujificha, lakini msako mkali uliofanywa uliwabaini na kukamata kundi la kwanza la watu 63 ambao walikaa sehemu ambayo gari haliwezi kufika.

“Baada ya kuwakamata wahamiaji hao haramu kundi la kwanza la askari waliendelea na msako ambapo waliwakamata wahamiaji wengine tisa waliokuwa wakijaribu kutaka kutoka kwenye pori hilo,” aliongeza Kamanda Shana.

Alisema wahamiaji hao haramu wanatarajiwa kukabidhiwa Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya hatua za kisheria pamoja na mfanyabiashara aliyekamatwa anayetuhumiwa kuwasafirisha.

XS
SM
MD
LG