Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:05

Maelfu ya wa-Libya hupoteza maisha yao wakielekea ulaya


Wahamiaji wa Libya wakiwa kwenye boti wakielekea ulaya
Wahamiaji wa Libya wakiwa kwenye boti wakielekea ulaya

Kila mwaka maelfu ya wahamiaji wa kiafrika wanaondoka Libya wakiwa wamepanda boti chakavu na kuhatarisha maisha yao wakisafiri kwenda kutafuta fursa nzuri huko Ulaya. Wahamiaji wengine wengi wanabaki katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, wakivutiwa na fursa mbali mbali lakini pia wakikumbwa na kutendewa vibaya katika mikono ya wafanya magendo na wasafirishaji haramu wa binadamu.

Libya kwa muda mrefu imewavutia wahamiaji wanaosaka maisha bora. Lakini changamoto za kiusalama ambazo hazijapatiwa ufumbuzi, zimedhoofisha miundo mbinu na kushusha thamani ya sarafu na hivyo kupelekea hali mbaya za maisha na maamuzi yasiyo ya kawaida kwa wahamiaji wengi ambao wanajikuta wakiishi huko.

Wahamiaji wa Libya katika bahari ya Mediterranean. Jan. 15, 2018.
Wahamiaji wa Libya katika bahari ya Mediterranean. Jan. 15, 2018.

Othman Belbeisi ni mkuu wa tume isiyo ya kiserikali ambayo inafanya kazi kwa ajili ya uhamiaji salama. Katika mahojiano yake na Sauti ya Amerika-VOA alisema kwamba Libya siku zote imekuwa ni kituo cha muda kwa wahamiaji, lakini utawala mbaya, miundo mbini iliyochakaa na changamoto za kiuchumi zinawazuia wahamiaji kuwa na njia mbadala na pia hali ya ukosefu wa sheria inachangia. Hiyo imepelekea kile ambacho Belbeisi anakiita “utumwa mambo leo,” ambapo watu wanashikiliwa bila ya ridhaa yao na kulazimishwa kujiingiza katika hali ambazo zinatishia maisha yao.

Libya ni mwenyeji wa kiasi cha wahamiaji 700,000 kutoka nchi 35, Belbeisi alisema. Baadhi yao ndiyo kwanza wamewasili, lakini wengi wengine wameishi nchini humo kwa miaka kadhaa. Wamefika hapo wakiwa na matarajio tofauti. Baadhi yao wanapanga kufanya kazi. Wengine wana azma ya kubaki kwa muda mfupi nchini humo, kabla ya kugundua kwamba hawana njia za kusonga mbele. Wengi ni kutoka Afrika Magharibi na wengi hawana hati halali za kusafiria.

XS
SM
MD
LG